Naibu Waziri, Ofisi Ya Rais, Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Deogratius Ndejembi Amesema Kuna Ulazima Wa Halmashauri Kutenga Maeneo Mahususi Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Shule Ili Kukidhi Mahitaji Yanayotokana Na Ongezeko La Wanafunzi Ikiwa Ni Pamoja Na Kutatua Changamoto Za Wanafunzi Kutembea Umbali Mrefu.
Ndejembi Ametoa Wito Huo Akiwa Mkoani Dar Es Salaam, Wakati Wa Ziara Yake Ya Kikazi Ya Kukagua Ujenzi Wa Miundombinu Ya Elimu Inayojengwa Kupitia Mradi Wa Boost Na Sequip Katika Halmashauri Ya Jiji La Dar Es Salaam Na Halmashauri Ya Manispaa Ya Kinondoni.
Ndejembi Amesema Maeneo Hayo Yakitengwa, Kuna Ulazima Wa Kujenga Shule Za Ghorofa Badala Ya Majengo Ya Chini Ili Kutatua Changamoto Ya Kukosa Viwanja Vya Michezo Vya Watoto Ambavyo Ni Muhimu Kwa Ajili Ya Kujenga Afya Ya Akili.
“Michezo Ni Muhimu Kwa Ajili Ya Afya Ya Akili Na Makuzi Ya Watoto Hivyo Ni Lazima Kuwepo Na Ushirikiano Wa Viongozi Kuanzia Ngazi Ya Mtaa, Kata, Halmashauri, Wilaya Na Mkoa Katika Kuhakikisha Shule Zinajengwa Kwenda Juu Ili Kupata Maeneo Ya Viwanja Vya Michezo,” Amesema Ndejembi.