Takriban Wapalestina 400 wameuawa na mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza, ndani ya muda wa saa 24 zilizopita, kulingana na maafisa wa afya wa Palestina, na 60 waliuawa katika mashambulizi ya usiku.

Israel ilishambulia maeneo ya makazi ya watu huko Gaza, ikiwa ni pamoja na kambi ya wakimbizi ya Jabalia yenye watu wengi, na maeneo karibu na hospitali za Al-Shifa na Al-Quds za Gaza.
China imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano Gaza, na kusema kuwa itafanya chochote kinachohitajika kukomesha ghasia hizo.



