Barabara kadhaa nchini Uganda zitafungwa kupisha sherehe za siku ya kuzaliwa Rais Yoweri Museveni ambaye anaadhimisha miaka 79, sherehe ambazo zitakazofanyika katika Uwanja wa Uhuru leo Septemba 8, 2023.
Sherehe hiyo iliyoandaliwa na vijana, wakiongozwa na Mratibu wa Kitaifa katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha National Resistance Movement (Chama Tawala), Hadijah Uzeiye Namyalo, inatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 100,000 kutoka nchi mbalimbali.
Licha ya sherehe hiyo kufanyika leo, siku ya kuzaliwa ya Rais Museveni itaadhimishwa Septemba 15, 2023 ambayo ndio tarehe aliyozaliwa Rais huyo.