NCHIMBI KUZUNGUMZA NA WANANCHI SHINYANGA AKISAKA KURA ZA CCM

Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Septemba 3, 2025 amewasili mkoani Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya kampeni ya kusaka kura za chama hicho katika nafasi za uraisi ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Dkt. Nchimbi amefanya mikutano miwili akianzia wilayani Kishapu ambapo amenadi  sera na ilani ya chama hicho katika kiwanja cha SHIRECU kilichopo mjini Mhunze na kisha kuendelea na utaratibu wa kunadi sera za chama hicho katika uwanja wa Jasco uliopo katika kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga ambapo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 Oktoba na kukichagua  chama cha mapinduzi.

Aidha Balozi nchimbi ameainisha miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali ya chama cha mapinduzi katika kipindi cha awamu ya sita kwa mkoa wa Shinyanga kuwa ni pamoja na ujenzi na upanuzi wa kiwanja cha ndege kilichopo katika kata ya Ibadakuli  manispaa ya Shinyanga pamoja na ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, vituo vya afya pamoja na shule za msingi na za sekondari

Lakini pia Nchimbi ameanisha miradi wanayotarajia kuitekeleza  katika kipindi cha siku 100 endapo watafanikiwa kuingia madarakani katika uchaguzi huo  kuwa ni pamoja na  suala la bima ya afya kwa watu wote katika makundi ya wazee, watoto, walemavu na wanawake wajawazito.

Katika mkutanohuo, Nchimbi pia amewanadi Wabunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini  Patrobas Katambi, Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu,  Lucy Mayenga, pamoja na mgombea wa  Jimbo la Solwa  Ahmed  Salum  wakati katika jimbo la  Itwangi amemtambulisha  Azza Hillal Hamad pamoja na wagombea wa udiwani katika kata za mkoa wa Shinyanga.

Kwa siku tarehe 4 September Balozi Nchimbi ataendelea kuinadi   Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030 wilayani Kahama ambapo asubuhi anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara katika miji ya Isaka na Kagongwa na kisha saa sita mchana atazungumza na wananchi katika kiwanja cha parking ya malori karibu na uwanja wa taifa uliopo katika manispaa ya Kahama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *