CEO wa Records label ya Konde Gang na Staa wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize ‘Konde Boy’ leo ameandika ujumbe ambao umetafsirika umeenda kwa wasanii waliowahi kuwa Konde Gang.
Harmoniz kupitia instagram ameandika ‘harmonize_tz CHINGA HIS BACK!!!!! @ibraah_tz Nimekaa Hapa Nawatazama Wale Waliofanikiwa Kuwatia Ujinga Wasanii Wengine Ambao Walikuwa @kondegang Na Kuwaaminisha Watafanikiwa Zaidii Hata Mimi wakati Mwingine Ilinibidi Niamini Hivyo Ndiomaana Kwa Moyo
Mkunjufu Nilizibariki Safari Zaoo!!! Ila Chakusikitisha IMEKUWA SIVYO NDIVYO !!’
‘Busara Unyenyekevu Uvumilivu Nibaadhi Ya Vitu Vinamfanya CHINGA Awe Hapa Leo!!!! PROUD OF YOU BROTHER ushauri Wako Naufanyia Kaziii Ingawa Nilikaribia Kukata Tamaa Kabisa Kuwa Support Wasanii Wengine lla MANENO YAKO YAMENIPA NGUVU UPYA!!!! 2 MEMBERS @kondegang HUU MWAKA !!! 2024
© Mtag Msanii Unaemuona MKALI ILA HAJAPATA Nafasi!’ – Harmonize