Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Navalny amemtuhumu Rais Vladimir Putin kwa mauwaji ya mumewe

Mke wa kiongozi wa upinzani wa Russia Alexei Navalny amemtuhumu Rais Vladimir Putin kwa mauwaji ya mumewe na ameahidi kutaja majina ya wale anaodai walihusika na kifo chake.

Tuhuma hizo zimetolewa baada ya mamake Alexei, Lyudmila kusema kuwa amezuiliwa kuuona mwili  wakijana wake kwa siku ya tatu mfululizo.

Ila Ikulu ya Kremlin ikisema kuwa wanaufanyia uchunguzi  mwili huo kutokana na kifo chake .

Kifo cha Navalny akiwa kwenye gereza moja ya Russia wiki iliopita kimeshtua viongozi wa upinzani wa Russia waliokimbilia mataifa ya kigeni, pamoja na mataifa ya magharibi, wakati kidole cha lawama kikielekezwa kwa Kremlin.

Yulia Navalny Jumatatu amekutana na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Charles Michel mjini Brussels, baada ya kutoa tuhuma zake dhidi ya Putin na baada ya waziri wa mambo ya nje wa Ujeruimani Annalena Baebock, kusema kwamba atapendekeza vikwazo vipya dhidi ya Moscow kutokana na kifo cha Navalny

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *