Nauli zapanda, wanafunzi kuendelea kulipa sh.200

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) leo Novemba 27, 2023 imetangaza nauli mpya za daladala kwa safari ndefu na fupi katika maeneo ya mijini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habib Sauo nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600

Kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 550 sasa itakuwa shilingi 700,Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi shilingi 900.

Safari ya kilometa 26 hadi 30 nauli ni shilingi 1100, safari ya kilometa 31 hadi 35 ni shilingi 1300 na kilometa 36 hadi 40 nauli ni 1400.

Aidha nauli za wanafunzi zitaendelea kusalia 200 kwa safari za masafa mafupi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *