Nani kuwa Rais wa DRC, Tshisekedi au Katumbi?

Rais wa DRC Félix Tshisekedi na mpinzani wake Moïse Katumbi ndio wagombea ambao wameorodheshwa katika nafasi ya juu katika uchaguzi ambao umepangwa kufanyika mwezi ujao huku wawili hao wakiwa wameimarisha kampeni zao kwa kuzuru zaidi ya mikoa mitano kuelekea uchaguzi wa Disemba 20.

Wiki moja tu baada ya kampeni rasmi kuanza nchini Drc, vitengo vitano vya wagombea mbalimbali vimechipuka kuhusiana na jinsi ambavyo wanaendesha kampeni zao.

Wagombea wawili, rais Félix Tshisekedi na Moise Katumbi, wamejitambulisha kwa raia kwa mtindo wa kutumia rasilimali muhimu kufanya kampeni.

Rais Tshisekedi ambaye anawania urais kwa muhula wa pili tayari amefanya kampeni zake katika mikoa ya kinshasa alipozindua kampeni yake, Kongo-Central, Maniema, Équateur Na Ubangi Kaskazini.

Aidha mpinzani wake Katumbi ambaye kampeni yake inaangazia kurejesha amani, uboreshaji wa kijamii na ujenzi wa kitaifa amefanya kampeni katika mikoa sita ya Tshopo, Kivu Kusini, Haut Na Bas-Uele, Ituri Na North Kivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *