Mke wa marehemu Mohbad, Cynthia Omowumi-Aloba, amedai kuwa anajua vitu vingi ila ana hofu ya kuuwawa na watu waliosababisha kifo cha mumewe.
Mama huyo wa mtoto mmoja ameandika kupitia Instastory yake na kudai kuwa waliotesa mumewe walimnyamazisha kwa kueneza uvumi kwamba alikuwa akitumia dawa za kulevya.