Taarifa zilizopo muda huu ni kuwa Jeshi la polisi nchini Nigeria limewashikilia watu wawili wanaotajwa kuhusishwa na kifo cha msanii Mohbad kilichotokea Septemba 12 mwaka huu.
Watu hao walioshikiriwa ni msanii Naira Marley na Promota Sam Larry na watakaa rumande kwa muda wa siku 21 kwa mahojiano zaidi na usalama wao pia.