Naira Marley na Sam Larry waachiwa huru

Azeez Fashola, maarufu  Naura Markey na Samson Erininfolami Balogun maarufu kama Sam Larrywameachiwa huru na Jeshi la Polisi Lagos, Nigeria, baada ya kutimiza masharti ya dhamana, siku ya jana Ijumaa jioni Novemba 17, baada ya kutimiza masharti ya dhamana.



Mahakama huko Yaba, Jimbo la Lagos imewaachia huru, Baada ya Jumatatu, Novemba 6, 2023, kutangazwa kwa dhamana yao ya Naira milioni 20 zaidi ya TZS milioni 59.

Naira Marley na Sam Larry kwa pamoja walikamatwa na kufikishwa mbele ya Mahakama kwa tuhuma za kuhusika katika kifo cha Mohbad, msanii wa zamani wa lebo ya Naira Marley, ambaye alifariki katika mazingira yenye utata mwezi Septemba 12.

Hakimu Adeola Olatunbosun aliwataka watuhumiwa kuwasilisha pasipoti zao na ameamuru wawasiliane kila wiki na Idara ya Uchunguzi wa Jinai ya Jimbo, Panti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *