
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Kundo Marthew ameziagiza Mamlaka za maji kote nchini,kukabiliana na tatizo la upotevu na wizi wa maji ili kupunguza gharama za uendeshaji wa miradi hiyo.
Akikagua na kuzindua mradi wa maji wa Manyamanyama-Mgaja uliopo wilayani Bunda mkoani Mara, Mhandisi Kundo amezitaka mamlaka kudhibiti upotevu wa maji huku akiipongeza mamlaka ya maji Bunda (Buwasa) kwa kuweka mikakati ya kubadili mita zisizofaa.
Katika hatua nyingine Naibu waziri Kundo,amezungumnzia umuhimu wa mradi wa maji taka unaotekelezwa wilayani Bunda ambao unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 7.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Bunda,Ester Gilyoma amesema Mamlaka hiyo ipo katika mpango wa kufanyia maboresho miundombinu yote ya utoaji maji huku baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo wakishukuru serikali inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zinazoendelea za kumtua mama ndoo kichwani.
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew amefanya ziara ya siku 2 Mkoani Mara kwa lengo la kukagua,kuzindua na kujionea hali ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi.