KAHAMA
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Zainabu Katimba amesema miradi yote kwa Manispaa ya Kahama itatekelezwa kwa jumla ya Shilingi Bilioni 27.4
Waziri huyo tarehe 4,Desemba alishuhudia Hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Stend ya Mabasi eneo la Mbulu,Soko la Sango pamoja na Ujenzi wa Stend ya Mabasi madogomadogo na Soko la Wajasiriamali eneo la Zongomela iliyofanyika katika eneo linalotarajiwa kujengwa stendi kuu Mbulu kata ya Muhongolo.
Waziri Katimba amesema kutajengwa vizimba,Migahawa na maeneo ya kupumzikia pamoja kituo cha polisi hivyo hawana mashaka na mkandarasi aliyesaini mkataba na utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Disemba 2024 hadi Disemba 2025
Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Tarura Humprey Kanyenye akisoma taarifa ya namna ya utekelezaji wa Miradi ya TACTIC alisema miji 45 inatekeleza miradi hiyo na imegawanywa katika makundi Matatu lengo la kuwepo mradi ni kuboresha miundombinu mbalimbali Kwa Kahama Mradi unatiwa saini leo ukikamilika utaongeza mapato kutoka shilingi Milioni 11 hadi kufikia shilingi Milioni 31.
Mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba amesema leo wamekuja kushuhudia utiaji saini Mkataba kwani wanashida na barabara mji unapanuka na watu wanaongezeka.
“Ngoja niseme Waziri huyu mkandarasi mliyempa kujenga barabara tangu alivyosaini mkataba amekuwa wa kusuasua alikuwa na greda moja kwenye eneo la kazi alivyoona unakuja ameongeza greda hivyo hatufai au serikali imsimamie kwa kumsukuma ili kazi iendelee” amesema Kishimba.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga amesema mradi huo ni wakanza kutekelezwa kwa Manispaa ya Kahama hivyo aliomba watakao tekeleza wakandarasi watumie vibarua wazawa na watumie uzalendo wa kutochelewesha Mradi.