MZOZO WA DRC: KAGAME, TSHISEKEDI WAKUTANA QATAR

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, imearifu kuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame na Félix Tshisekedi wa DR Congo wamekutana mjini Doha, Qatar na kukubaliana kuendelea na mazungumzo kuhusu mzozo unaondelea baina ya mataifa hayo na kutafuta amani ya kudumu.

Mkutano wao na Amir wa Qatar Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani, una dhamira ya kuleta upatanishi na kwa pamoja walikubali kuendelea kutafuta amani.

Umoja wa Mataifa, DRC na baadhi ya nchi za Magharibi zinaishutumu Rwanda kwa kuaqwaunga mkono wapiganaji wa M23 ambayo mara zote imekuwa ikikanusha madai hayo, lakini si safari hii.

Kwa mara ya mwisho, Kagame na Tshisekedi waliketi pamoja kuzungumzia suala hilo Septemba 2022 jijini New York Nchini Marekani wakiwa na mpatanishi wao Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *