Na William Bundala,Kahama
Wafanyabiashara katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameishukuru kampuni ya Jambo Food Products kwa kuwasogezea huduma karibu kwa kufungua duka la jumla la bidhaa Jamukaya hali itakayowapunguzia gharama na muda wa kusafiri kufuata bidhaa hizo Mkoani Shinyanga.
Wakizungumza na Jambo Fm baadhi ya wafanyabiashara wamesema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupata huduma kwa wakati kwani wakati mwingine wanapotafuta bidhaa kwenye maduka mengine wanakosa bidhaa hizo kutokana na mahitaji kuwa makubwa kuliko upatikanaji kwa wakati.
Ridhiki Hamis na Irene Massawe ambao ni wafanyabiashara katika Soko la Namanga wamesema kuwa kabla ya kufunguliwa kwa duka hilo walikuwa wanasumbuka kupata huduma kwa mawakala na kwamba uwepo wa duka la Jambo Kahama utawanufaisha kibiashara kwa kuwa na mzunguko mkubwa.
Kwa upande wake Meneja mauzo wa kampuni ya Jambo tawi la Kahama Emmanuel Maganga amesema kuwa wameamua kusogeza bidhaa za jambo karibu kwakuwa wateja wengi wa Kahama walikuwa wanasumbuka kufika Shinyanga na kuongeza kuwa bidhaa zote zinauzwa kwa bei ya kiwandani.
Sambamba na hayo Maganga ameongeza kuwa katika duka la jumla la Jambo lililofunguliwa Kahama kuna bidhaa za aina mbalimbali zinazopatikana zikiwemo soda mpya zenye ujazo wa milimita 500 pamoja na biskuti zenye ladha saba tofauti na kuongeza kuwa mteja anaponunua bidhaa za Jambo anapewa huduma ya usafiri bure.
Duka la jumla la bidhaa za Jambo Manispaa ya Kahama linapatikana Kahama mjini barabara ya Isaka mkabala katika jengo la Mkeni Plaza.
One response to “Mzigo umefika,umepokewa Kahama”
Nataman kuwa wakala wa hivyo vinywaji vipi napaye mwongozo?