TANZIA: Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ALI HASSAN MWINYI amefariki dunia leo February 29,2024 akiwa anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam.
Taarifa imetolewa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho Machi mosi.