Mwili wa Mtanzania Abraham Mgowano aliyekuwa akiishi Mareklani na kufanya kazi katika Kampuni ya Google kama Mhandisi wa Programu Endeshi (Software Engineer) umepatikana ukielea katika Mto Miami jijini Florida baada ya kuanguka toka kwenye Boti (Yacht)

Abraham aliripotiwa kupata ajali Februari 24, 2024 akiwa na wenzake 12 pamoja na Kapteni wa Boti hiyo.

Polisi walianza kuutafuta mwili huo bila mafanikio hadi walipopata taarifa za kupatikana kwa mwili huo ukielea jana Februari 27, 2024.