Mwili wa msanii Mohbad kufukuliwa

Jeshi la polisi kupitia Msemaji wake Kikanda wa Jimbo la Lagos, Benjamin Hundeyin amesema kuwa mwili wa msanii #mohbad ambaye alifariki Jumanne ya wiki hii, huenda ukafukuliwa ili kusaidia uchunguzi.

Kauli hiyo imeteoka wakati akifanya mahojiano na mwanahabari, Daddy Freeze, ambapo anabainisha kuwa italazimika kufanya hivyo ilikubaini kifo cha staa huyo aliyezikwa Jumatano hii kwani kifo chake kinatajwa kuwa na utata pamoja na maswali mengi hivyo watatakiwa kujua nini kilipelekea kufariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *