Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwili wa Askari aliyegongwa na gari waagwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (SACP) Wilbrod Mutafungwa hii leo amewaongoza mamia ya waombolezaji wakiwemo askari wa vyeo mbalimbali, maafisa wakaguzi, pamoja na ndugu wa marehemu kuaga mwili wa askari wa jeshi la polisi sanjenti, Stella Alfonce aliefariki kwa kugongwa na gari.

Sanjenti Stella alifariki Novemba 1 2023 katika eneo la Nyamhongolo jijini Mwanza wakati akitekeleza majukumu yake baada ya kugongwa na gari ya shule ya msingi nyamuge iliyopo jijini mwanza.

Ibada ya kuaga mwili wa askari huyo imefanyika katika kanisa katoliki kigango cha Isegenghe Parokia Ya Nyakato Jijini Mwanza ambapo makundi mbalimbali yameshiriki kuuaga mwili wa askari huyo.

Akiwasilisha salamu za rambirambi kamanda Mutafungwa amesema uhai wa stella ulitoweka akiwa anafanya kazi ya kusimamia sheria barabarani.

Mwili wa Stella umesafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya Maziko ambayo yanatarajiwa kufanyika kesho Novemba 3, mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *