Msanii wa muziki Maua Sama kupitia wakili wake Claudio Msando wamemfungulia kesi mwanamtandao na mtangazaji Mwijaku kwa kosa la kumuandika vibaya mtandaoni Mauasama.

Wakili wa Maua Sama Claudio Msando kutoka kampuni ya Mawakili na Wanasheria ya Msando Law Office wamemuandikia Mwijaku hati ya madai na kumpa muda wa saa 24 ya kujibu tuhuma hizo ikiwemo kumuomba radhi na kumtaka kumlipa fidia ya kiasi cha Shilingi Milioni Mia Tatu na endapo Mwijaku akishinwa kufanya hivyo basi atafikishwa Mahakamani


