Mwigizaji wa Squid Game, kwenda jela kwa kosa la Unyanyasaji wa Kingono

Mwigizaji wa filamu ya “Squid Game,” kutoka Korea Kusini, Oh Young-soo(79), amehukumiwa kifungo cha miezi minane jela na kifungo nje cha miaka miwili, kwa kumnyanyasa kingono mwanamke mwaka 2017.

Mzee Oh Young -Soo alishtakiwa kwa kosa la kumkumbatia na kumbusu shavuni mwanamke ambaye alikuwa akitemba barabarani mnamo mwaka 2017.
Na mwanawake huyo alifungua mashtaka dhidi ya Oh mnamo Desemba 2021, baada ya mwigizaji huyo mzee kupata umaarufu kwa upande wake katika filamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *