Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwenyekiti ampiga na kumjeruhi mhudumu wa baa baada ya kumdai  sh. 24,000

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Mapya wilayani Tarime, Silas Nyamhanga (46), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Tarime-Rorya kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mhudumu wa baa, Jenipher Shaban.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Marck Njera amesema chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kudaiwa Sh.24,000 alizokunywa pombe katika baa hiyo, ambapo mtuhumiwa alimhadaa mwanamke huyo na kumpeleka nyumbani kwake ili akamlipe, badala yake alimfungia ndani ya uzio na kuanza kumshambulia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *