Mwenye umri wa miaka 70 ajifungua mapacha

Raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 70 amekuwa mwanamke mkongwe zaidi barani Afrika kujifungua, huku hospitali moja katika mji mkuu wa Uganda Kampala ikitangaza kuzaliwa kwa mapacha ambao wote ni wazima.

Safina Namukwaya alijifungua mvulana na msichana siku ya Jumatano kwa njia ya upasuaji baada ya kupata mimba kupitia In Vitro Fertilization (IVF), Kituo cha Kimataifa cha Hospitali ya Wanawake na Uzazi huko Kampala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *