Mwenye Miaka 65 Anafanya Kazi Gani Mtaani Kwako?

Na Ibrahim Rojala

Leo hii imetimia miaka 65 tangu kuzaliwa kwa kocha la makombe na Mkufunzi matata kabisa wa Real Madrid, Carlo Ancelotti aliyezaliwa 10 Juni 1959 huko Reggiolo, Italia.

Hadi sasa takribani Makocha 20 wamebeba kombe la UEFA Champions League zaidi ya mara moja, kati yao wanne tu wameweza kubeba zaidi ya mara mbili

Mwamba Carlo Ancelotti peke yake ndiye ameweza kushinda taji la UEFA Champions League mara tano na aliweka rekodi hiyo mwaka huu kwenye Uwanja wa Wembley Juni 1,2024 Real Madrid ilipoichapa Dortmund mabao 2-0.

Ancelotti pia ni miongoni mwa makocha sita pekee walioshinda kombe hilo wakiwa na timu nyingi, na mmoja kati ya saba ambao walioshinda makombe hayo kama wachezaji na baadae kushinda kama makocha.

Katika Umri wa Kustaafu Ancelloti ndio kwanza Ni Kama Vile anaanza kazi rasmi kulingana na namna anavyokisuka Kikosi cha Real Madrid.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *