MWENGE WA UHURU WATUA SIMIYU, KUKAGUA NA KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO

Na Saada Almasi – Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha leo Agosti 9, 2025 ameupokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Njiapanda Wilayani Maswa Mkoani Simiyu.

Macha ameupokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita tayari kwa kuukimbiza katika Halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kesho kufikishwa wilayani Meatu na baada ya kuzindua miradi kadhaa ya kimaendeleo unatarajiwa kuelekea wilaya ya Itilima kisha Bariadi na hatimaye Wilayani Busega.

Ukiwa Mkoani Simiyu, Mwenge wa Uhuru utazindua, kufungua, kuweka mawe ya Msingi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 25.9.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *