Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Halmashauri ya Mji Babati iliyopo Mkoani Manyara, hii leo Julai 15, 2025 imepokea Mwenge wa Uhuru kutoka katika Halmashauri ya Wilaya Babati Vijijini.
Akipokea Mwenge huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, CPA Shaaban Mpendu amsema Mwenge huo wa Uhuru utatembelea jumla ya Miradi nane yenye thamani ya Shilingi Bilion 3.3 ikiwemo Afya, Elimu, maji, Utawala na Maendeleo.

Mpendu amesema Mwenge huo utakimbizwa kwa kilometa 105.7 ambapo mbali na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pia ripoti ya Viwanja vya Michezo itatolewa.







