MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA KILOMETA 1,230 KAGERA

Na Cecilia Shiratu, Bukoba – Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhan Kido amesema, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa mkoani Kagera Agosti 30, 2026 Wilayani Muleba, ukitokea Mkoa wa Geita, ambapo utakimbizwa katika Halmashauri nane, umbali wa kilomita 1,230.

Mwenge huo, utatembelea, kuzindua, kufungua, kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 54 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 23.07.

RC Kido ameeleza kuwa, miradi hiyo imejikita katika sekta ya afya, maji, elimu, miundombinu, nishati, uwezeshaji wa vijana kiuchumi, mazigira wezeshi kwa wawekezaji na uhifadhi wa mazigira.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhan Kido.

Ujumbe mkuu wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2026 unahusu, Amani, Umoja na mshikamano wa kitaifa Chini ya kauli mbiu isemayo, “Tanzania ni yetu sote tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo”

Aidha, Mwenge huo wa uhuru utaendelea kuhamasisha na kuelimisha Wananchi juu ya mapambano zidi ya Rushwa, Malaria, VVU, Dawa za Kulevya na uzingatiaji wa lishe Bora.

Mwenge huo wa uhuru unatarajiwa kukamilisha mbio zake mkoani Kagera Septemba 6, 2026 na utakabidhiea Mkoani Kigoma Septemba 7, 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *