MWENGE KUTEMBELEA MIRADI YA BILIONI 139,926,901,532.42 MANYARA

Na Afarah Suleiman, Mererani – Manyara.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Halima Dendego leo 12/07/2026 amepokea Mwenge wa Uhuru 2026 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makala katika Uwanja wa Soko la Getini Mji Mdogo wa Mirerani kata ya Mirerani.

Mwenge wa Uhuru 2026 katika Mkoa wa Manyara utakimbizwa kwa siku saba katika Halmashauri Wilaya ya Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang na Mbulu.

“Mwenge wa Uhuru Ukiwa mkoani Manyara utazindua, Kuweka mawe ya Msingi na Kutembelea jumla ya miradi ya maendeleo 49 yenye thamani ya Bilioni 139,926 901,532.42. Na kukimbizwa kwa kilometa 1371.70,” alielekeza Dendego.

Mwenge wa Uhuru 2026 unatarajiwa kupokelewa tarehe Julai 15 2026 katika Halmashauri ya Mji Babati na kutembelea miradi ya Maendeleo 7 yenye thamani ya Bilioni 8,076,843,781.12 kati ya miradi hiyo 3 itazinduliwa 2 itawekewa mawe ya Msingi na 2 kutembelewa kwa jumla ya kilometa126.7 kuanzia mapokezi na kukabidhi.

Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 ni “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *