Watu saba wamefariki dunia wakiwemo Wanakwaya waliokuwa wakisafiri kutoka Chome kuelekea Ndolwa wengine 75 kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti ya ajali zilizotokea Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro,.
Katika ajali ya kwanza, yenyewe ilitokea majira ya saa saba usiku eneo la Njoro ikihusisha basi la Osaka lililosababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 52 walijeruhiwa.

Ajali ya pili ni ile iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster iliyotokea majira ya saa 2 asubuhi baada ya kupinduka katika kona za milima ya Ilamba, na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi 23.
Baadhi ya majeruhi wa ajali iliyotokea usiku wamesema ilisababishwa na mwendokasi, hali iliyomfanya dereva kushindwa kulimudu gari, huku chanzo cha ajali ya pili kikihusishwa na hitilafu ya mfumo wa gari.

Kufuatia ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amewasihi madereva kuwa waangalifu, huku akiwataka abiria kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapobaini hali yoyote inayoweza kuhatarisha usalama wao.


