MWANZA YAHAMASISHA MATUMIZI MIFUMO YA KIBENKI KUKUZA UCHUMI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana, amezitaka taasisi za kifedha zilizopo ndani ya Mkoa huo hususani za Benki, kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kibenki kwa njia ya simu, ili kuchochea ukuaji wa uchumi katika jamii.

Balandya ameyasema hayo wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 22 wa Shule ya Kibenki Tanzania (TIOB), ulioandaliwa kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambapo amesema maendeleo ya Teknolojia yameleta mabadiliko chanya katika sekta ya fedha, hivyo ni wajibu wa mabenki na taasisi za fedha kuwasaidia wakulima na wafugaji kutumia njia hiyo rahisi kukuza shughuli zao.h

Amesema, Wananchi wa Mwanza zaidi ya asilimia 75 wanajishughulisha na kilimo huku asilimia 7 wakifanya uvuvi kama shughuli kuu za uchumi hivyo ni lazima kuwafikia waliko kwa kidijiti ili kuhakikisha wanatumia muda wao kwenye uzalishaji wakiwa wanafanya miamala kwa simu.

Katika hatua nyingine  Balandya pia ametumia jukwaa hilo kutoa wito kwa washiriki wa mkutano huo na wananchi wote kwa ujumla kujiandaa kupiga kura kwa uhuru na amani kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba ya Gavana wa Benki Kuu, Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu, Dkt. Nicas Yabu amesema wanaendelea kutoa kozi fupi na muhimu kwa watoa huduma wa  sekta ya fedha  ili kuwajengea uwezo  huku wakizingatia viwango vya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *