Mahakama kuu mjini Kigali imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela mwandaaji wa shindano la Miss Rwanda Ishimwe Dieudonne maarufu kama Prince Kid kwa kosa la ubakaji na kuomba rushwa ya ngono.
Mnamo Aprili 2022 Kid alikamatwa baada ya kubainika kuwa alihusika katika unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya washiriki wa Miss Rwanda kwa miaka 10 chini ya usimamizi wake kama Mkurugenzi Mtendaji wa Rwanda Inspiration Back Up inayoandaa shindano hilo.