MWANANCHI MUSOMA ACHUKULIWA NA WATU WASIOJULIKANA.

Na Adam Msafiti-Mara.

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Burungu halmashauri ya wilaya ya Musoma mkoani Mara aitwaye Herman Juma (45) mfanyabiashara na mvuvi anaripotiwa kuchukuliwa na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake na kisha kutokomea naye kusikojulikana.

Aidha Jeshi la Polisi mkoani Mara limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pius Lutumo, amesema mtu huyo alikamatwa tarehe 14 Februari mwaka huu na watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa usalama wakiwa na gari la kiraia na kisha kuondoka naye.

Kamanda Lutomo amesema”Watu hao wakiwa na gari la kiraia waliondoka na mtu huyo na hadi sasa hajulikani aliplekwa kituo gani,kutokana na taarifa hiyo Jeshi la Polisi mkoa wa Mara lilianza uchunguzi mara moja ili kubaini ukweli wa taarifa hiyo lakini pia kubaini chanzo cha tukio hilo”.

Bi Pendo Turutumba ambaye ni mke wa mtu huyo anayedaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana,ameeleza kuwa mumewe hakuwa na uhasama na mtu yeyote hapo kijiji kwao huku akiomba Jeshi la Polisi kusaidia kupatikana kwa mumewe.

“Mimi siku hiyo nilimuaga mume wangu kuwa nakwenda kutafutia maisha watoto wangu muda si mrefu akanifuata mtoto akaniambia mama unaitwa, ndio nikaenda mpaka kwa Mwenyekiti wa kitongoji akaniambia hao watu wamekuja wakasema wao ni usalama wa Taifa,inamaanisha wenyewe ni maaskari.” Amesema Bi Pendo.

Mwenyekiti wa kitoji cha Burungu senta Bw.Matibabu Mbogora anaeleza kuwa yeye kama mwenyekiti wa eneo hilo aliwaona watu hao ambao walimwamuru kumpigia simu Afisa mtendaji wa kijiji cha Bukumi na alipofika alifanya nao mahojiano na baadaye hakujua kilichoendelea mpaka pale walipoamua kuondoka.

Aidha kufuatia tukio hilo baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Burungu senta na kijiji cha Bukumi kwa ujumla wameingiwa na hofi,huku wakisema eneo lao Halima matukio ya kushangaza ya namna hiyo ambapo wameomba msaada wakufanikisha kupatika kwa mwanakijiji mwenzo akiwa salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *