Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwanamke ajifungua mtoto akiwa katika kituo cha mabasi

Mwanamke mmoja, amejifungua mtoto akiwa katika kituo cha mabasi katika Jiji la Lagos, Nigeria na kushangiliwa na umati wa watu waliokuwa wamekusanyika karibu na eneo hilo.

Maofisa wa huduma za dharura wameiambia BBC kuwa Mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa alikuwa akisubiri kupanda basi kwenye Kituo cha Mabasi cha Onipanu wakati alipopata uchungu wa kujifungua ghafla.


Kwa mujibu Shirika la Usimamizi wa Dharura la Jimbo la Lagos (Lamesa) Wafanyabiashara wa kike katika soko lililopo eneo hilo ndio waliogeuka wakunga, wakambeba hadi mahali penye utulivu na kumsaidia kujifungua mtoto wa kiume, na wakapelekwa hospitalini.


Habari za mwanamke huyo zimeteka mitandao ya kijamii Nigeria, baadhi wakipendekeza majina mbalimbali kwa ajili ya mtoto huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *