Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwanafunzi afariki akiwa anafua nguo za shule bwawani


Mwanafunzi wa Darasa la saba  Katika  shule ya Msingi Mbabani iliyopo kata ya Mtakuja Halmashauri ya mji Wa aliyefahamika kwa jina la Dominanti Masumbuko mwenye umri wa miaka 13 amefariki dunia baada ya kuangukia bwawani wakati akifua nguo zake za shule.

Baadhi ya mashuhuda wamesema tukio hilo wakati mwanafunzi huyo  anafua nguo zake za shule kwa bahati mbaya aliteleza hadi kwenye bwawa hilo akaanza kuogelea kwa lengo la kujiokoa lakini maji yakamzidi nguvu hali iliyopeleka umauti.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita Mrakibu Hamis Dawa amesema mtoto huyo alifariki kwenye bwawa hilo ambalo awali lilikuwa linatumika kuchimba moramu kwa ajili ya ujenzi wa barabara na jeshi hilo lilifika na kuokoa mwili wa mtoto huyo ambaye tayari alikuwa ameshapoteza maisha.

Kamanda Dawa ametumia nafasi hiyo kuwasihi wazazi na walezi Mkoani Geita kuchukua tahadhari za kutosha katika kuwalinda watoto wao kuacha kucheza ama kufanya shughuli yoyote kwenye mabwawa kama ama sehemu ambapo maji yanatumaa hasa katika kipindi cha mvua zinazoendelea kunyesha ili kujiepusha na matukio kama hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *