Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Hassan Iddi Mwamweta (Balozi Mteule) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani. Bw. Mwamweta anachukua nafasi ya Balozi Abdallah Saleh Possi ambaye amehamishiwa Geneva, Uswisi.
