MWALIMU WA KUJITOLEA MBARONI KWA KOSA LA KUMBAKA MWANAFUNZI MWANZA.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia Paul James ambae ni mwalimu wa kujitolea katika shule ya msingi Nyangomango kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita (13) katika shule ya msingi Nyangomango wakati akijisomea masomo ya ziada katika maktaba ya shule hiyo.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 23.12.2024 majira ya saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano alfajiri huko katika kijiji cha Nyangomango kata ya Ntende wilaya ya Misungwi mkoa wa  Mwanza ambapo inadaiwa mwalimu huyo alimbaka  binti huyo ambae jina lake limehifadhiwa bila ridhaa yake na mpaka sasa jeshi hilo linamshikilia kwa hatua zaidi za kisheria.

Katika hatua nyingine Mutafungwa pia amesema jeshi la polisi katika mkoa huo pia linamshikilia Charles Manyanda (19) mkazi wa kijiji cha Mwasagila kata ya Misasi wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza kwa kosa la kumuua babu yake anaitwa Charles Kasela (62) kwa kumpiga na kitu butu katika sehemu mbalimbali za mwili wake ambapo chanzo cha mauaji hayo ni mtuhumiwa huyo kuugua ugonjwa wa afya ya akili.

Aidha kamanda mutafungwa amesema jeshi la polisi katika mkoa huo linaendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yote ya mkoa huo na kwa wale wote ambao watabainika kukiuka sheria na taratibu za nchi bas hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *