Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwalimu Jela Maisha kwa kumlawiti mwanafunzi wake

Mwalimu wa Shule ya Msingi St Mathew iliyopo Kongowe, Livingston Kyarwenda (40) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka tisa.

Hukumu hiyo imetolewa leo, Novemba 29, 2023 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Herieth Mwailolo, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Kyarwenda, mkazi wa Mbagala Chamanzi anadaiwa kumlawiti mwanafunzi huyo wa kiume aliyekuwa anasoma darasa la nne katika vyoo vilivyopo shuleni hapo.

Hakimu Mwailolo amesema kutokana na uzito wa ushahidi wa mashahidi watano uliotolewa mahakamani hapo ukiwemo ushahidi wa mtoto mwenyewe, mahakama hiyo imeridhika pasi na kuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa ulitenda kosa hilo kinyume cha sheria na kuongeza kuwa mshtakiwa ana haki ya kukata rufaa iwapo hajaridhika na hukumu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *