Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwalimu amdhalilisha  mwanafunzi  wake na kumnywesha sumu kupoteza ushahidi

Polisi wilayani Bunda mkoani Mara wanamshikilia Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Masahunga iliyopo wilayani humo kwa tuhuma za kumdhalilisha mwanafunzi wake na kisha kumnywesha sumu ili kupoteza ushahidi.

Mwanafunzi huyo wa kike mwenye umri wa miaka 16 anasoma darasa la sita katika shule hiyo na tukio hilo lilitokea Machi 09, 2024 majira ya saa tatu usiku nyumbani kwa mwalimu mkuu huyo kwenye Kijiji cha Kisorya.

Akisimulia mkasa huo Mama wa mwanafunzi huyo amesema siku ya tukio binti yake hakurudi nyumbani na alibaki kwa mwalimu huyo Ili kusaidia kazi za nyumbani kwani mke wa Mwalimu huyo ambaye ni ndugu yake alikuwa safarini, na kuongeza kuwa  ilikuwa ni kawaida kwa binti yake kulala nyumbani kwa Mwalimu huyo kutokana na kuwa ndugu.

Mama huyo amedai kuwa alipokea taarifa za binti yake kuonekana eneo tofauti na nyumbani kwa Mwalimu huyo huku akiwa na hali mbaya na walipofika eneo la tukio walimchukua na kumpeleka kituo cha Afya cha Kisorya na kisha kuhamishiwa hospitali teule ya Bunda, ambapo Vipimo vya awali vya madaktari vimeonyesha kuwa binti huyo amedhalilishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *