Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwakinyo hatopanda Ulingoni Kesho

Bondia Hassan Mwakinyo amesema hatopanda ulingoni katika pambano lake na raia wa Namibia, Julius Indongo lililopangwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.

Mwakinyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema hatoweza kupanda ulingoni kutokana na uongo na udanganyifu wa ‘Mapromota’ wa pambano hilo.

“… naomba niweke hisia zangu wazi kwa mashabiki ya kuwa kesho sitaweza kupanda ulingoni kutokana na wongo na udanganyifu, wa ma promota,” ameandika Mwakinyo.

Aidha, bondia huyo ametaka kutatuliwa kwa changamoto hiyo leo kama waandaaji wanataka pambano hilo lifanyike.

Hata hivyo Bondia huyo , mapema leo alipima uzito na mpinzani wake kuelekea pambano hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *