Bondia Hassan Mwakinyo amesema kuwa amebadilishiwa mpinzani kwenye pambano lake la Septemba 29 huku akitoa sababu ya kutokea kwa jambo hilo.
”Napenda kuwataarifu mashabiki zangu ya kuwa kumetokea mabadiliko kidogo juu ya kubadilishiwa mpinzani na hii ni baada ya bondia okwiri kurusha chu…. na hii ni baada ya kuchomoa game Binafsi sijaridhishwa na mabadiliko haya lakini ni bora kugawa chakula kilicho kwisha andaliwa kuliko kutupa…natumai washabiki zangu ni waungwana na kwa pamoja mtaelewa mabadilko haya.”- ameandika Hassan Mwakinyo

Mwakinyo sasa atapigana na Julius Indongo raia wa Namibia tarehe hiyo 29 Septemba 2023.