Mvua zasababisha Wanafunzi zaidi ya 300 Kuhamishwa Ushetu

 Zaidi ya wanafunzi 300 wa Shule wa Shule ya Msingi Igwamanoni Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamelazimika  kuhamishwa baada ya madarasa matano waliyokuwa wakiyatumia kupata nyufa na kutitia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Athari za Mvua hizo zimeikumba kata ya Igwamanoni hususani katika Vijiji Luhaga na Igwamanoni ambapo baadhi ya Nyumba zimepata nyufa na kubomoka.

Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Kahama ikiongozwa na mkuu wa wilaya Hiyo Mboni Mhita imetembelea baadhi ya nyumba kujionea athari za mvua hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Hadija Kabojela amesema kuwa Tofauti na athari zilizotokea kwenye shule hiyo zaidi ya kaya 500 katika vijiji vya Luhaga na Igwamanoni zimepata maafa kutokana na mvua hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *