Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amewataka Wananchi kuchukua tahadhari na kuhifadhi chakula, kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa mvua za El Nino.
Silinde ameyasema hayo hii leo Agosti 26, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Nancy Nyalusi aliyeuliza ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya Wakulima.

Akijibu Swali hilo, Silinde amesema, “nitoe rai kwa Wananchi kuwa tumesikia taarifa zimetolewa na Mamlaka za Hali ya Hewa Nchini na Duniani kuhusu uwepo wa utabiri wa mvua za El Nino kwa mwaka huu,”
“Kama kutakuwa na El Nino, kutakuwa na changamoto katika uzalishaji na kama kutakuwa na changamoto katika uzalishaji maana yake tunaweza kuwa na hatari kubwa ya uwepo wa njaa katika mwaka unaofuatia, hivyo tutunze chakula.” amesema Silinde.


