‘MV SERENGETI HAIJAZAMA BALI IMETITIA UPANDE MMOJA’ – TASHICO.

Kampuni ya meli Tanzania (TASHICO) imekanusha taarifa zilizokua zikisambaa mtandaoni zikidai meli ya MV. Serengeti imezama katika gati la bandari ya Mwanza kusini taarifa ambazo kampuni hiyo imedai kua sio za kweli kwani meli hiyo imetitia upande wa nyuma na sio kuzama kama inavyoelezwa.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) Alphonce Sebukoto amesema usiku wa kuamkia tarehe 26.12.2024 walipokea taarifa kua meli hiyo imetitia upande wa nyuma ambapo baaada ya kufika katika eneo hilo walibaini kua ilikua imeingiza maji ndani na baada ya hapo walianza hatua za kuiinua zoezi ambalo linaendelea mpaka sasa.

Sebukoto amesema toka mwaka 2016 meli hiyo imekua haifanyi kazi na ilikua imeegeshwa ikisubiri matengenezo makubwa na katika kipindi hicho ilikua ikiangaliwa na wataalamu na siku tatu hapo nyuma wataalamu hao walikua wametoka kuiangalia.

Katika hatua nyingine Sebukoto pia amesema meli hiyo ni moja kati ya meli ambayo ina faida kwa serikali kwani ina uwezo wa kubeba zaidi ya watu 500 na taki 250 za mizigo na ilikua katika mpango wa kufanyiwa matengenezo katika bajeti ya 2025/2026 na endapo matengenezo yake yatakamilika itakwenda kua msaada mkubwa kwani inauwezo wa kuhudumia maeneo ya visiwani nah ii ni kupitia milango yake ambayo inarushusu kusimama sehemu yoyote na watu wakaingia ndani hivyo ni meli nzuri kwa abiria wa vijijini katika maeneo ambayo hakuna miundombinu ya bandari.

Aidha pia amesema wakiwa kama chombo cha usafirishaji kwa sasa wapo katika mpango wa kuimarisha hali ya ufuatiliaji wa mifumo ya kiusalama ikiwemo ufungaji wa kamera na alamu za kisasa ili kubaini viashiria vyovyote ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama.

Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mwanza Said Sekibojo amesema mpaka sasa hakuna madhara yoyote ambayo yamepatika katika chombo hicho na upo uwezekano mkubwa wa kukinyanyua na endapo zoezi hilo litafanyika kadri ya matarajio yao basi mpaka kufikia jioni ya leo watakua wamekiinua.

Tukio hili linakuja ikiwa miezi kadhaa imepita tangu tukio la meli ya Mv Clarius iripotiwe kuanguka upande katika ziwa Victoria tukio ambalo lilitokea tarehe 19.05.2024 ambapo mpaka sasa bado uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *