Muuza duka ashiriki kutupa mtoto chooni

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Shinyanga limethibitisha kuwakamata watu wawili Kufuatia picha ya video iliyosambaa mitandaoni Ikimuonyesha mtoto mchanga aliyefariki dunia Akielea katika tundu la choo, Ambao majina yao hayajawekwa wazi kwa sababu ya Upelelezi wakazi wa kata ya Lyabukande halmashuari ya Ya Shinyanga.

Watu hao wamekamatwa kwa tuhuma za kutoa mimba akiwemo binti Aliyetoa mimba hiyo na muuzaji wa duka la dawa Aliyefanikisha tukio hilo.

Akizungumza na Jambo Fm kamanda wa jeshi la polisi mkoa Wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema tukio hilo Limetokea tarehe Septemba 12 2023 majira ya saa nne usiku ambapo binti huyo anayesoma kidato cha Nne katika shule ya sekondari Lyabukande alipata Ujauzito na hakutaka wazazi na walimu wajue suala hilo.

Magomi ameongeza kuwa Mwanafunzi huyo alimshirikisha muuzaji wa duka la dawa ambae Alimpa vidonge na kuvinywa kisha ujauzito huo ukatoka na kumtupa mtoto huyo chooni.

Katika hatua nyingine kamanda magomi amewaasa vijana Kufuata mila na desturi za mtanzania na kuacha tamaa Ambazo zinaweza kuwaangiza katika mambo yasiyofaa na Wajielekeze zaidi lkatika elimu ili wafikie ndoto zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *