Muonekanao wa lips za mrembo kutoka Kenya, Tanasha Donna ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa muziki Diamond Platnumz umezua gumzo mtandaoni ambapo Tanasha anadaiwa kufanya upasuaji mdogo wa urembo ili kukuza lips zake.

Mbali na muonekano huo pia Tanasha amewahi kutajwa kufanya upasuaji(Plastic Surgery ) ili kuongeza shape yake (Umbo lake la Mwili).
Mrembo huyo anaingia kwenye orodha ya mastaa kutoka Afrika Mshariki waliofanya upasuaji wa midomo yako ambao ni pamoja na mwanamitandao Malaika Cute na Nicole Berry.