Mume wa Diva – Sina ndoa hadi muda huu

Mume wa Diva ambaye ni Mtangazaji wa Wasafi,  Abdulrazak salum Mubarak ameweka wazi kuwa hadi wakati huu hana ndoa nyingie zaidi ya hii ya Diva ambayo alifungwa mwanzoni mwa mwaka 2022.

Abdulrazak amefunguka hayo huku pakiwa na shutuma za kuwa na mke mwingine, kitendo kinachotafrisiwa kuto mfurahisha mrembo huyo ambaye siku chache nyuma aliwema kuanzia sasa hayupo kwenye ndoa.

SOMA UJUMBE WA MUME WA DIVA:Vitu vyote Vizuri kwenye Huu Ulimwengu wabaki navyo ila waniachie wewe mtanga wangu Only You, wewe ndio Ninaekupenda. Sijawahi kukutana na mwanamke strong kwenye maisha yangu kukuzidi wewe, nimekukosea saana ukanisamehe, maneno mengi umeyasikia na kuambiwa bado ukanisamehe, mengi umeyaona na bado ukanisamehe, Kukulinda ni jukumu langu hata iweje. Kokote ulipo Nataka wewe ujue na Dunia Ijue Sina ndoa hadi muda huu zaidi ya ndoa yangu na wewe, na kama Mume katika ndoa Hii NIMEKURIDHIA radhi zangu unazo na kama Pepo ni radhi za mume basi tayari pepo yangu unayo. NITAKULINDA na NITAKULINDA, vita zako zote niachie mimi NITAPAMBANA nazo hata kama zinatoka ndani ya familia yangu MIMI nitapambana nazo. @divatheebawse You came during the darkest points of my life and you made it shine ✨, Letting you down is the worst thing I could do for myself”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *