Muimbaji wa Injili ahukumiwa kifungo

Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile (39), baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani Tu”, amehukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kosa la kuendesha Huduma ya Kiroho bila kibali

Wakili Boniphace Mwabukusi amesema “Kweli amehukumiwa lakini Mchungaji alifuata machakato wa kuomba vibali japo Serikali ndio ilikuwa ikichelewesha. Pia, Sheria inasema mtu ambaye yupo katika mchakato wa maombi hawezi kushtakiwa.”

Ameongeza “Adhabu aliyofungwa nayo ina faini na kifungo, Hakimu ametoa adhabu ya kifungo bila faini. Tunatarajia kukata rufaa Jumatatu (Oktoba 2, 2023).”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *