Muigizaji Kevin Hart aitembelea Rwanda

Mchekeshaji na mcheza sinema maarufu duniani kutoka Marekani, Kevin Hart aitembelea Rwanda kwa mujibu wa Gazeti maarufu la nchini Rwanda The New Times limedokeza.

Mchekeshaji huyo daraja A jumanne ya wiki hii alionekana kubarizi katika maeneo ya Haute Baso jijini Kigali akiwa na familia yake.

Baadaye maduka hayo makubwa jijini Kigali yalichapisha picha kwenye ukurasa wa Twitter wa maduka hayo wakimshukuru mchekeshaji huyo na mkewe kwa kuemea katika maduka yao.

Hart alijipatia umaarufu wake kutokana na kutokea katika jarida la came to ‘Undeclared’ kama mgeni mashuhuri huku umaarufu wake wa awali ilikuwa ni pale alipoigiza katika filamu ya ‘Paper Soldiers’, na kupaa Zaidi katika filamu zilizofuatia kama vile ‘Soul Plane’, ‘The 40-Year-Old Virgin’, ‘Death at a Funeral’ na ‘Little Fockers’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *