Mtunzi wa tamthilia kutoka Afrika Kusini, Mbongeni Ngema amefariki dunia kwa ajali ya gari familia yake imethibitisha.
Kabla ya umauti Mbongeni ametengeza filamu mbalimbali ikiwemo ya Sarafina! ambayo iliyoigizwa na Whoopi Goldberg mnamo 1992 ambapo pia ilipata mafanikio ya kimataifa na iliteuliwa kwa Tuzo za Tony na Grammy.
Filamu ya Sarafina! Alisimulia ambavyo mwanafunzi alikuwa akipigana dhidi ya ubaguzi wa rangi.