MTUCHAGUE TUIFANYIE SHINYANGA MAMBO MAKUBWA ZAIDI – DKT. SAMIA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Mgombea Urais wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Shinyanga, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mikutano ya kampeni, akinadi sera na kuomba kura kwa mikoa ya kanda ya ziwa, huku akiwahimiza Wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Mkutano huo wa Kampeni, umefanyika hii leo Oktoba 11, 2025 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga, ambapo Dkt. Samia aliwanadi Wagombea Ubunge na Madiwani wa Majimbo saba ya Uchaguzi Mkoani Shinyanga, akisema kwamba kipindi cha miaka minne tangu aingie madarakani serikali imefanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na miradi ya maendeleo na ile ya kimkakati na kwamba anaomba ridhaa ya wanachi ili awe kukamilisha miradi mingi Zaidi.

Amesema, “tulipofika hapa ni miradi mingi ambayo tumeitekeleza na kama mnavyojua maendeleo ni hatua hivyo kipindi cha miaka minne iliyopita tumepiga hivyo tunaitaji miaka mingine mitano zaidi ili tuendelee kupiga hatua.”

Aidha Dkt. Samia amepokea maombi na changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wagombea Ubunge hao na kusema anakwenda kuzifanyia kazi, huku akiwakabidhi ilani ya CCM ya 2025-2030 ya miradi ya maendeleo inayopaswa kutekelezwa katika mkoa wa Shinyanga.

Naye mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega mjini ambaye pia Waziri wa Kilimo, Husein Bashe akizungumza katika mkutano huo amewaasa wananchi kuichagua CCM, kwani wanakwenda kukifufua chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ili kiweze kijuiendesha na kuinua uchumi wa wakulima.

“Niwaeleze wana Shinyanga tunakwenda kulipa madeni yote yanayokikabili chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU)ili chama hicho sasa kiweze kujiendesha kwa kununua pamba na kuuza nje ya nchi,“ amesema Bashe.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Pangani ambaye pia Waziri wa Maji, Juma Aweso ameainisha baadhi ya miradi ya maji iliyotekelezwa na Serikali katika Wilaya ya Kishapu na Ushetu – Kahama, akisema watakapoichagua CCM, dhamira ni kuhakikisha vijiji na vitongozji zaidi katika mkoa wa Shinyanga vinaunganishwa na mradi wa maji wa ziwa Victoria.

Nao baadhi ya wananchi walioudhuria mkutano mkutano huo, akiwemo Amina Salum mkazi wa Kata ya Ndala na Hania Njile mkazi wa Kata Mjini Manispaa ya Shinyanga wameelezea matarajio yao kuwa ni kuona ahadi alizotoa Dkt. Samia zinatekelezeka atapochaguliwa kuwa rais wa Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *